Uzinduzi wa Kituo cha Tiba ya Afya cha AYUSH

Balozi wa India apa nchini Sandeep Arya amezindua kituo cha tiba ya afya kiutumia dawa za asili na mazoezo ya viungo katika Kituo cha utamaduni wa India kwa lengo la kueneza tiba hiyo hapa nchini hatua ambayo itasaidia katika kukinga visababishi vya magonjwa.

 Balozi wa India apa nchini - Sandeep Arya (pili kushoto) na Mkurugenzi wa Taasisi ya dawa za jadi  Dk Easter Innocent (pili kulia) wakizindua kituo hicho


Balozi Arya amesema tiba hiyo ijulikanayo kiini cha habari ya AYUSH kinashugulika na mifumo ya AYUSH ikiwemo tiba ya afya, tiba ya ustawi, dawa za asili za India pamoja na tiba ya kisaikolojia, kimwili na kiroho jamba ambalo amesema linaunga mkono urithi wa mfumo wa dawa za kihindi ambazo kwa sasa zinatumika na watu wengi wa jamii hiyo.

            Baadhi ya dawa za tiba ya jadi zilizotumika kwenye uzinduzi huo Jijini Dar es Salaam

                           Mkurugenzi wa Taasisi ya dawa za jadi - Dk Easter Innocent

Pia Mkurugenzi wa Taasisi ya dawa za jadi Dk Easter Innocent amesema serikali ya Tanzania kwa sasa inatambua umuhimu wa dawa za asili licha ya kuwepo kwa imani potofu miongoni mwa jamii ya matumizi ya dawa hizo huku baadhi yao wakifananisha na ushirikina, lakini pia ameongeza kuwa endapo serikali itaboresha sera na mikakati tasnia hiyo itaweza kufanya kazi zake kwa ufanisi zaidi.


Uzinduzi wa Kituo cha Tiba ya Afya cha AYUSH Uzinduzi wa Kituo cha Tiba ya Afya cha AYUSH Reviewed by Unknown on September 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Chips Mayai Ni Hatari Kwa Afya Yako

Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo...

Powered by Blogger.