Kampuni ya Sokabet Imezinduliwa Rasmi Jana



Kampuni ya Sokabet imezinduliwa rasmi jana ambapo itakuwa inajihusisha na michezo ya kubashiri matokeo (kubet) ambayo nia yake kubwa ni kuwawezesha Watanzania kupata fedha, kukuza michezo na kuchangia maendeleo mbalimbali ya kijamii.




 Kampuni hiyo ya Kitanzania yenye maskani yake jijini Dar es Salaam itawawezesha washiriki kubashiri matokeo kupitia tovuti yake ya www.sokabet.co.tz ambapo washiriki wanaweza kuvuna fedha nyingi hadi shilingi milioni 100 kwa kubet kwa shilingi 1,000 tu.

Licha ya Sokabet kuwawezesha washiriki wenye umri wa kuanzia miaka 18 kubet pia inayo nafasi ya kukuza michezo kwa kuwekeza katika taasisi mbalimbali mfano kwa kuanzia imeanza na Klabu ya Majimaji ya Ruvuma.

Sokabet inakuwa mmoja wa wadhamini wa Majimaji, klabu inayoshiriki katika Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo itatoa mamilioni ya shilingi katika ufadhili huo ikiwa ni sehemu ya kurejesha kile inachokipata kwenye jamii.

 Mshambuliji wa Kimataifa aliyewahi kutamba pia na timu ya Taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa anaitumikia timu ya MajiMaji ya Songea Danny Mrwanda, ametamba kwamba baada ya klabu yao kupata udhamini mnono wa milioni 150, kutoka Soka Bet sasa wao ni kucheza Kandanda ili kupata matokeo.

Kauli hiyo ameitoa wakati viongozi wa klabu yake walivyokuwa wakisainiana mkataba wa kudhamini klabu yao kwa mwaka mmoja ,ambapo mekiri sasa ,kazi iliyobaki ni kusakata kandanda pekee Uwanjani.

Nyota huyo aliyewahi kung'ara zaidi kimataifa ,amesema kikosi cha Maji Maji msimu huu kimeandaliwa vyema na wapo katika kuhakikisha wanapambana katika,Ligi Kuu ya Tanzania Bara hadi kieleweke.
 




Kampuni ya Sokabet Imezinduliwa Rasmi Jana Kampuni ya Sokabet Imezinduliwa Rasmi Jana Reviewed by Unknown on September 04, 2017 Rating: 5

No comments:

Chips Mayai Ni Hatari Kwa Afya Yako

Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo...

Powered by Blogger.