Na Ally Killasama.
Vijana wengi wa karne hii wametawalwa na tatizo la
kuwa na kitambi na baadhi ya jamii zetu nyingi hasa kutoka bara la Afrika,
kumejengeka dhana kuwa kitambi au unene huashiria utajiri, ishara ya ufanisi au
mafanikio. Ugonjwa wa kitambi huweza kuwakumba watoto, vijana, watu wazima na
hata wazee wa jinsia zote.
Kitambi ni tumbo kubwa ambalo huchomoza kwa mbele ya
tumbo na wakati mwingi kuning’inia isivyo kawaida. Huu ni ugonjwa kama magonjwa
mengine na unaweza kutibika na pia siyo hivyo tu bali pia historia ya magonjwa
katika fani ya elimu afya jamii inatueleza kuwa ugonjwa huu unaweza kutibika.
Mwili wa binadamu una seli bilioni 50 mpaka 200 za mafuta zilizogawanyika mwilini.
Kwa wanawake zipo sana maeneo ya matiti, nyonga, kiunoni na kwenye makalio, Kwa
wanaume seli hizo zipo sana kwenye kifua, tumboni na kwenye makalio. Katika
mwili wa binadamu kuna unene wa aina kuu mbili, kwanza ni ule unaosababishwa na
kutozingatia kanuni na taratibu za lishe bora inayojulikana sana kama (balance
diet) kwa mfano kula vyakula vyenye kiasi kikubwa cha mafuta na wanga kama
viazi ya kukaanga (chips),mafuta ya kupikia hasa yale yatokanayo na bidhaa za
wanyama kama vile siagi, pizza, vyakula vyenye wanga mwingi kama ugali wa
mahindi, mihogo, wali, mikate mweupe na pia viazi mviringo, nyama n.k pia
unywaji wa mara kwa mara wa pombe kama vile bia pamoja na kutofanya mazoezi ya
mwili. Mafuta ya tumbo yanayofanya kitambi hukusanywa kwa njia kuu mbili, ya
kwanza ni mafuta kutoka kwenye tishu zilizo chini ya ngozi na ya pili ni kutoka
kwenye ogani za ndani kama moyo, pia tatizo kitambi mara nyingine huwa ni ule
unaotokana na urithi kutoka kwa wazazi au ukoo pia kuna sababu za kimazingira
na nyingine zisizojulikana.
Picha ya muonekano wa mtu mwenye kitambi jinsi mafuta yanavyoganda
Kuna matatizo mbali mbali yanayo ambatana na kitambi.
Mosi, madhara ya kiafya kama vile ugonjwa wa moyo, shinikizo la damu, kisukari
aina ya pili (diabetes type II). Pili, madhara ya kisaikolojia, hasa pale mtu
anapojishuku kupoteza mvuto. Hali imeshamiri sana hasa katika nchi zilizoendelea
ambapo watu huchukulia unene au kitambi kama ulemavu fulani wa kimwili.
Njia za kuepuka na kupunguza kitambi.
Kufanya mazoezi ya mwili kila siku kwa dakika 30-60
walau siku 4 au 5 kwa mfano kukimbia, kuluka kamba, kuendesha baiskeli na
kufanya kazi kwa uwingi.
Kuzingatia mlo mzuri kiafya, huu ndio ufunguo wa
kupunguza na kuepukana na kitambi. Kuacha kula vyakula vinavyotia nguvu sana,
vyenye mafuta na sukari ya kupitiliza ndio njia ya kuondoa kitambi. Hii
husaidia mwili kutumia mafuta yaliyo mwilini kutengeneza nguvu hivyo kupunguza
mafuta na kuondoa kitambi. Aidha, punguza matumizi ya vinywaji vyenye sukari
kwa wingi na tumia samaki badala ya nyama.
Kufanya upasuaji mkubwa ili kupunguza mafuta, hii
hufanyika kwenye nchi zenye teknolojia kubwa kama India na Malekani, kitendo
hichi hushauriwa endapo mafuta yaliyomwilini yamesababishwa na magonjwa
yameshindwa kupungua kwa njia ya rahisi ya kawaida.
Iringa yetu ilifanya mahujiano na Dk. Boniface Bruno
Mwero ambae yupo katika kitengo cha tiba kutoka kituo cha NEEMA REHABILITATION
mkoani Iringa na kuelezea mengi kuhusu swala zima la ugonjwa wa kitambi na kati
ya hayo alieleza kuhusu adhari na tiba kwa watu wenye ugonjwa huo. Hizi ndio
adhari ya mtu mwenye kitambi
Udhaifu wa misuli, hii ni pale misuli badala ya
kubakia na seli za kuzalisha nishati au ngufu humpelekea mtu ile sehemu ya
misuli inaanza kuchukuliwa na mafuta, utakuta mtu analalamika maumivu ya mgongo
ni kwasababu hakula uwezo wa ushirikiano kati ya misuli ya mbele na misuli ya
mgongoni.
Kuongezeka kwa uzito, mtu anakuwa
hawezi kuimili mwili wake na inafika kipindi shindikizo la damu kuweza kupanda,
pia hali hii upelekea mafuta kuifadhiwa katika mishipa ya damu zinaanzakujaza
mafuta na kusababisha matatito kama kisukari na kiharusi (strock).Wengi huchukia kitambi lakini kuna
wenye mapenzi nacho kama Bw. Ismail Swaleh mkazi wa Gangironga na kusema yeye
kwake ni heshima kuwa na kitambi“kuna kipindi nilikua sina kitambi
na watu waliniona ni mtu wa kawaida ata nikiwa na pesa kiasi gani, lakini
sahivi nimepata kitambo yaani naheshimika na kila mtu na kuonekana mtu mwenye
pesa zangu” akisema hayo Bw. SwalehPia Dk. Mwero aliongezea na kutoa tiba kwa
wale wanaosumbuliwa na ugonjwa wa kitambi na hizi ndio tiba za ugonjwa huo.Ili kuondoa kitambi inabidi kuchoma
mafuta yaliyo hifadhiwa katika misuli na njia bora ni kufanya mazoezi kwa
wingi. Kupunguza vyenye wanga au mafuta
mengi na kula vyakula vyenye vitamini na protini ili mwili ulazimike kubadilisha
yale mafuta kuwa kama chanzo cha nishati. Pia unywaji wa maji (vuguvugu) mengi husaidia
tatizo hili na kusaidia kuwa na uwiano wa vimiminika katika mwili.
Baadhi ya vyakula na matunda mbalimbali yenye kujenga Afya mwilini.
Kitamaduni kwa hapa Tanzania mtu
mwenye kitambi huonekana ni mtu mwenye uwezo kipesa wakati ni ugonjwa
mbaya sana na wa kuepukika na kitaalamu humpelekea mtu kuwa na magonjwa kama
ugonjwa ya moyo, shindikizo la damu n.k lakini watu hawalioni hilo na kukaazana
na magojwa mengine kama Maleria. Kuwa na uzito uliozidi sio kuwa na kitambi
kwasababu uzito unachangiwa na mifupa, misuli, wingi wa damu na vimiminika
mwilini.
KITAMBI NI MAUMBILE AU UGONJWA?
Reviewed by Unknown
on
May 03, 2018
Rating:

No comments: