Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo la damu,kisukari na saratani za aina zote.
Sahani moja ya chips kavu huwa na mafuta yanayokaribia nusu kikombe cha chai ambayo ni sawa na ujazo wa mililita 250. Kwahiyo walaji wengi wa chips wapo katika hatari ya kutengeneza sumu kwenye miili yao bila kujua.
Utafiti unaonyesha watu wengi hupendelea kula chips mayai, kuku, soseji au hata kwa mishikaki maana yake ni kwamba kiwango hicho cha nafuta huzidi kwa sababu na vyenyewe huwa vimekaangwa. Jambo la kusikitisha ni kwamba wafanyabiashara wamekuwa hawazingatii umuhumu wa kutumia mafuta mara moja katika kukaanga vyakula hivyo. huwa wanapikia mafuta kwa zaidi ya mara mbili na hivyo kuzidisha hatari zaidi.
“Wanazidisha hatari kwa saba kawaida mafuta yanapaswa kupikiwa mara moja. Kadri unavyounguza mafuta ndivyo ambavyo ule mfumo wa mafuta masafi ambayo yanatakiwa kwa mwili wa mwanadamu unabadilika na kuwa machafu, maana yake ni kwamba unapopikia mafuta zaidi ya mara mbili tayari yanakuwa yametengeneza sumu ambayo haitakiwi mwilini,”
Mafuta ambayo yametumika kukaangia vyakula zaidi ya mara mbili hubadilika na kutengeneza utandu mweupe ambao huweza kuonekana iwapo mtu atayatazama kwa macho yake. Ule utandu mweupe utakaouona unatoa ishara kwamba mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu, lakini wafanyabiashara huendelea kuyatumia bila kujali au pengine kutokujua kwamba wanaziweka afya za walaji katika hatari ya kupata magonjwa.”
Pamoja na kiwango hicho cha mafuta ambacho huingia mwilini kwa ulaji wa sahani moja pekee ya chips kavu mlaji hula chumvi nyingi iliyopo ndani ya nyanya maalumu iliyosagwa (tomato). Tomato jinsi ilivyotengenezwa ina chumvi nyingi, ulaji wa mafuta mengi jumlisha na chumvi nyingi na ninavyofahamu walaji wengi wa chips hupendelea kushushia na kinywaji chenye sukari kama vile Soda, maana yake unakuwa umetengeneza sumu ndani ya mwili wako.
Wengi hatuzingatii ulaji wa chakula bora, tunakula mradi tule na hatuzingatii kupima afya zetu.Wakati umefika tunapaswa tubadilike kwa sababu wagonjwa wanaongezeka. Utafiti unaonyesha kati ya watu 100 wenye umri wa miaka 25 na kuendelea, 9 kati yao tayari wanaugua ugonjwa wa kisukari. Kila mwaka duniani watu milioni 12 hugundulika kuwa wana saratani na asilimia 60% ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na mfumo mbovu wa maisha hasa ulaji usiofaa.
Wenzetu wazungu sio kwamba hawali chips, wanakula lakini wanazingatia ‘menu’ ya sahani wanayokula. Kwamba inakuwa na viazi kidogo, mboga za majani kwa wingi na matunda. Sisi kwetu ni kinyume Kabisa tunapendelea kutumia Tomato sauce kwa wingi. Ulaji wa mbogamboga ni jambo la msingi kwani huenda kusaidia kurahisisha mfumo wa umeng’enywaji wa chakula tumboni.
Chips Mayai Ni Hatari Kwa Afya Yako
Reviewed by Unknown
on
May 19, 2018
Rating:

No comments: