Utambulishaji wa Mkaa wa Brikwiti nchini Tanzania

Katika kusaidia kufanikiwa kwa agenda ya serikali ya kupunguza matumizi ya mkaa unaotokana kwa kukatwa kwa miti jumla ya wakina mama lishe 100 wamefanikiwa kupata elimu ya kutumia nishati ya mkaa ujulikanao kwa jina la Brikwiti utokanao na mabaki ya taka ikiwemo yatokanayo na mimea.

Teknolojia hiyo ya utengenezaji wa nishati mbadala imetambulishwa hapa nchini na taasisi kutoka Norway ya Norges Vel ambayo ilishirikiana na IMED Foundation ambao ndio wamesambaza elimu kwa akina mama hao lengo ikiwa ni kukabiliana na uharibu wa mazingira ambao umekuwa ukijitokeza kutokana na kasi ya ukataji miti ovyo kwa ajili ya kutengeneza mkaa na kuni huku kundi la mama lishe likitajwa kuongoza matumizi ya nishati hiyo.

                          Mkurugenzi wa IMED Foundation - DK. Donath Olomi 


                                 Msimamizi wa mradi wa Norges Vel - Neatness Bwege

Wakizungumzia teknolojia hiyo Msimamizi wa mradi huo Neatness Bwege na Mkurugenzi wa IMED Foundation DK. Donath Olomi wamesema licha ya nishati hiyo kupunguza uharibifu wa mazingira pia inapunguza gharama za matumizi wa mkaa wa utokanao na miti.

Mkaa awa Brikwiti hutengenezwa na mabaki ya mimea mikavu mfano, pumba za mpunga, malanda, maganda ya karanga, miwa ambayo husindikwa kwa kutumia mashine maalumu.

                 Mwenyekiti wa mama lishe mkoa wa Dar es Salaam Bi. Mwanahamisi Mwendero 

Pia Mwenyekiti wa mama lishe mkoa wa Dar es Salaam Bi. Mwanahamisi Mwendero amesema matumizi ya mkaa huo wa Brikwiti ni mazuri na unaweza kukaa na moto mpaka masaa 6 bila kuzima na pia ni mzuri kwa afya maana hauna moshi.


Utambulishaji wa Mkaa wa Brikwiti nchini Tanzania Utambulishaji wa Mkaa wa Brikwiti nchini Tanzania Reviewed by Unknown on September 18, 2017 Rating: 5

No comments:

Chips Mayai Ni Hatari Kwa Afya Yako

Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo...

Powered by Blogger.