MWANDISHI WA HABARI, MUHINGO RWEYEMAMU KUAGWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JANA JUMANNE SEPT 5, 2017


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe jana Septemba 5 amewasili na kuongoza waombolezaji katika mazishi ya Mwandishi wa habari mkongwe nchini, Muhingo Rweyemamu.


Muhingo ambaye alifariki dunia Jumapili kwenye Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, na zoezi la Kuaga miili ulifanyika kwenye Viwanja vya Mnazi mmoja, Dar es Salaam.



Mbali ya Dk. Mwakyembe, wengine walio hudhuria mazishi ya Muhingo ambaye pia aliwahi kuwa mkuu wa wilaya za Handeni, Makete na Morogoro ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wabunge na viongozi wa vyama vya siasa.





Mwili wa marehemu Muhingo uliagwa mapema katika kanisa la KKKT Mbezi, kisha kupelekwa katika viwanja hivyo, ambako pia risala mbalimbali zilitolewa kna waandishi mbalimbali na viongozi pia.

Mara baada ya kuagwa kwa miili wa marehemu uwanjani hapo, waombolezaji walielekea kwenye makaburi ya Kinondoni kwa ajili ya mazishi.

Katika uhai wake, marehemu Muhingo aliwahi kuwa mwalimu kabla ya kusomea na kuanza kazi ya uandishi wa habari ambako alitumikia vyombo kadhaa vikiwamo magazeti ya Mtanzania na Mwananchi.

MWANDISHI WA HABARI, MUHINGO RWEYEMAMU KUAGWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JANA JUMANNE SEPT 5, 2017 MWANDISHI WA HABARI, MUHINGO RWEYEMAMU KUAGWA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JANA JUMANNE SEPT 5, 2017 Reviewed by Unknown on September 06, 2017 Rating: 5

No comments:

Chips Mayai Ni Hatari Kwa Afya Yako

Ulaji wa chips umetajwa kuwa hatari kwa afya ya Binadamu, kwani husababisha maradhi mengi yasiyo ya kuambukiza hasa figo, moyo, shinikizo...

Powered by Blogger.