Prof. Lipumba: Sitawafukuza Wabunge wa Majimbo, ila Wakimsikiliza Maalim Seif Nitawaondoa wote
Jana Prof Lipumba alikuwa na sherehe ya kuwapokea wabunge wa viti maalumu katika ofisi za chama Buguruni. Mkusanyiko huo ulioruhisiwa na polisi ulihudhuriwa na wanachama wengi wa CUF.
Katika sherehe hiyo, akizungumza na waandishi wa habari Prof Lipumba amenukuliwa akisema "Sina nia ya kufukuza wabunge wa majimbo, lakini kama watakuwa na kiburi cha kumsikiliza Maalim Seif, basi wembe ni uleule."
Lipumba anasema ana vijana wake aliowafundisha siasa toka akiwa mwalimu Chuo Kikuu, akimtolea mfano mbunge wa Malindi-Zanzibar, Mh. Ally Salehe.
Prof Lipumba anasema wabunge wa majimbo, wasimsikilize Maalim Seif,akiwaita kwenye kamati ya Maadili ya chama, wafike haraka na sio kumsikiliza Maalim Seif ambaye atawaponza na kusababisha wao wapitiwe na wembe kama wa wale wabunge wa kuteuliwa ambao saizi wanajuta kwa kumsikiliza Maalim Seif, na sasa wameonja ubunge wa miaka miwili, huku wakiwa na madeni tele waliyokopa kwa kudhani watakaa bungeni miaka mitano.
Baadhi ya wabunge wa kuteuliwa, wamesema wanaingia kazini ili kuhakikisha CUF kinarudi kuwa chama kikuu cha upinzani, na katika maeneo watakayokuwepo, hakutakuwa na CHADEMA wala chama kingine cha upinzani kuibuka.
Lipumba amewaasa wabunge hao kuwa watii kwa viongozi wa chama, na watambue ofisi yao ipo Buguruni na sio sehemu nyingine.

Prof. Lipumba: Wakimsikiliza Maalim Seif Nitawaondoa wote
Reviewed by Unknown
on
September 17, 2017
Rating:

No comments: